Zaburi 136:13-26 NEN

Zaburi 136:13-26

136:13 Za 78:13Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu,

Fadhili zake zadumu milele.

136:14 Kut 14:22; Za 106:9Na kuwapitisha Israeli katikati yake,

Fadhili zake zadumu milele.

136:15 Kut 14:27Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu,

Fadhili zake zadumu milele.

136:16 Kut 13:18; Za 78:52Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa,

Fadhili zake zadumu milele.

136:17 Hes 21:23-25; Yos 24:8-11; Za 78:55; 135:9-12Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu,

Fadhili zake zadumu milele.

136:18 Kum 29:7; Yos 12:7-24Naye aliwaua wafalme wenye nguvu,

Fadhili zake zadumu milele.

136:19 Hes 21:21-25Sihoni mfalme wa Waamori,

Fadhili zake zadumu milele.

136:20 Hes 21:33-35Ogu mfalme wa Bashani,

Fadhili zake zadumu milele.

136:21 Kum 1:38; Yos 12:1; 14:1Akatoa nchi yao kuwa urithi,

Fadhili zake zadumu milele.

136:22 Kum 29:8; Za 78:55; Isa 20:3; 41:8; 42:19; 43:10; 44:1, 21; 45:4; 49:5-7Urithi kwa Israeli mtumishi wake,

Fadhili zake zadumu milele.

136:23 Za 78:29; 103:14; 115:12Aliyetukumbuka katika unyonge wetu,

Fadhili zake zadumu milele.

136:24 Yos 10:14; Neh 9:28; Kum 6:19Alituweka huru toka adui zetu,

Fadhili zake zadumu milele.

136:25 Mwa 1:30; Mit 6:26Ambaye humpa chakula kila kiumbe.

Fadhili zake zadumu milele.

136:26 Za 105:1; 115:3; Ezr 3:11Mshukuruni Mungu wa mbinguni,

Fadhili zake zadumu milele.

Read More of Zaburi 136