Zaburi 136:1-12 NEN

Zaburi 136:1-12

Zaburi 136

Wimbo Wa Kumshukuru Mungu

136:1 Za 105:1; 100:5; 145:9; 118:1-4; 106:1; Ezr 3:11; Hes 2:26; 1:7; 2Nya 5:13; Yer 33:11Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema.

Fadhili zake zadumu milele.

136:2 Za 105:1; Kum 10:17; Kut 18:11Mshukuruni Mungu wa miungu.

Fadhili zake zadumu milele.

136:3 Za 105:1; Kum 10:17; 1Tim 6:15Mshukuruni Bwana wa mabwana:

Fadhili zake zadumu milele.

136:4 Kut 3:20; Ay 9:10Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu,

Fadhili zake zadumu milele.

136:5 Mit 3:19; Yer 51:15; Mwa 1:1Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu,

Fadhili zake zadumu milele.

136:6 Mwa 1:1; 1:6; Isa 42:5; Yer 10:12; 33:2Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji,

Fadhili zake zadumu milele.

136:7 Mwa 1:14, 16; Za 74:16; Yak 1:17Ambaye aliumba mianga mikubwa,

Fadhili zake zadumu milele.

136:8 Mwa 1:16Jua litawale mchana,

Fadhili zake zadumu milele.

Mwezi na nyota vitawale usiku,

Fadhili zake zadumu milele.

136:10 Kut 4:23; 12:12Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,

Fadhili zake zadumu milele.

136:11 Kut 6:6; 13:3; Za 105:43Na kuwatoa Israeli katikati yao,

Fadhili zake zadumu milele.

136:12 Kut 3:20; Kum 5:15; 9:29Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa,

Fadhili zake zadumu milele.

Read More of Zaburi 136