Zaburi 135:13-21 NEN

Zaburi 135:13-21

135:13 Kut 3:15; Za 102:12Ee Bwana, jina lako ladumu milele,

kumbukumbu za fahari zako, Ee Bwana, kwa vizazi vyote.

135:14 1Sam 24:15; Ebr 10:30; Kum 32:36Maana Bwana atawathibitisha watu wake,

na kuwahurumia watumishi wake.

135:15 Ufu 9:20; Isa 2:8; 31:7; 37:19; 40:19; Yer 1:16; 10:5; Za 96:5Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu,

zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

135:16 1Fal 18:26Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,

zina macho, lakini haziwezi kuona;

135:17 Yer 10:14; Hab 2:19zina masikio, lakini haziwezi kusikia,

wala hakuna pumzi katika vinywa vyao.

Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,

vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.

135:19 Za 22:23Ee nyumba ya Israeli, msifuni Bwana;

ee nyumba ya Aroni, msifuni Bwana;

ee nyumba ya Lawi, msifuni Bwana;

ninyi mnaomcha, msifuni Bwana.

135:21 Za 128:5; 134:3; 1Fal 8:13; 2Nya 6:2Msifuni Bwana kutoka Sayuni,

msifuni yeye aishiye Yerusalemu.

Msifuni Bwana.

Read More of Zaburi 135