Zaburi 135:1-12 NEN

Zaburi 135:1-12

Zaburi 135

Wimbo Wa Sifa Kwa Mungu

135:1 Neh 7:73Msifuni Bwana.

Lisifuni jina la Bwana,

msifuni, enyi watumishi wa Bwana,

135:2 1Nya 15:2; Lk 2:37; Za 116:19ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya Bwana,

katika nyua za nyumba ya Mungu wetu.

135:3 1Nya 16:34; Za 119:68; 68:4; 92:1; 147:1Msifuni Bwana, kwa kuwa Bwana ni mwema,

liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza.

135:4 Kut 19:5; Kum 7:6, 7; 10:15; Mal 3:17; Tit 2:14Kwa maana Bwana amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe,

Israeli kuwa mali yake ya thamani.

135:5 Za 48:1; 145:3; Kut 12:12; 1Nya 16:25; Ay 21:22Ninajua ya kuwa Bwana ni mkuu,

kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.

135:6 Za 115:3; Dan 4:35; Mt 6:10Bwana hufanya lolote apendalo,

mbinguni na duniani,

katika bahari na vilindi vyake vyote.

135:7 Ay 5:10; Za 68:6; Isa 30:23; Amo 4:13; Yer 10:13; 51:16; Yoe 2:23; Zek 10:1; Kum 28:12; Mwa 2:6; Ay 28:25; 38:22Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia;

hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua

na huleta upepo kutoka ghala zake.

135:8 Kut 4:23; 12:12Alimuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,

mzaliwa wa kwanza wa wanadamu na wanyama.

135:9 Kut 7:9; Za 136:10-15Alipeleka ishara zake na maajabu katikati yako, ee Misri,

dhidi ya Farao na watumishi wake wote.

135:10 Hes 21:21-25; Yos 24:8-11; Za 44:2; 78:55; 136:17-21Aliyapiga mataifa mengi,

na akaua wafalme wenye nguvu:

135:11 Hes 21:21, 26, 33; Yos 12:7-24Mfalme Sihoni na Waamori,

Ogu mfalme wa Bashani

na wafalme wote wa Kanaani:

135:12 Kum 29:8akatoa nchi yao kuwa urithi,

urithi kwa watu wake Israeli.

Read More of Zaburi 135