Zaburi 132:1-18 NEN

Zaburi 132:1-18

Zaburi 132

Maskani Ya Mungu Ya Milele Katika Sayuni

Wimbo wa kwenda juu.

Ee Bwana, mkumbuke Daudi

na taabu zote alizozistahimili.

132:2 Mwa 49:24; Isa 49:26; 60:16Aliapa kiapo kwa Bwana

na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:

132:3 2Sam 7:2, 27“Sitaingia nyumbani mwangu

au kwenda kitandani mwangu:

132:4 Rut 3:18sitaruhusu usingizi katika macho yangu,

wala kope zangu kusinzia,

132:5 1Fal 8:17; Mdo 7:46mpaka nitakapompatia Bwana mahali,

makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

132:6 1Sam 7:2; 17:12; Yos 9:17; 18:1; 1Nya 13:5Tulisikia habari hii huko Efrathi,

tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara:132:6 Yaani Kiriath-Yearimu.

132:7 2Sam 15:25; Za 5:7; 122:1; 1Nya 28:2“Twendeni kwenye makao yake,

na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake;

132:8 Hes 10:35inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia,

wewe na Sanduku la nguvu zako.

132:9 Ay 27:6; Zek 3:4; Isa 61:3, 10; Mal 3:3; Ay 29:14Makuhani wako na wavikwe haki,

watakatifu wako na waimbe kwa furaha.”

Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako,

usimkatae mpakwa mafuta wako.

132:11 Za 89:3-4, 35; 1Nya 17:11-14; Mt 1:1; Lk 3:31Bwana alimwapia Daudi kiapo,

kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua:

“Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe

katika kiti chako cha enzi,

132:12 2Nya 6:16; Za 25:10; Lk 1:32; Mdo 2:30kama wanao watashika Agano langu

na sheria ninazowafundisha,

ndipo wana wao watarithi

kiti chako cha enzi milele na milele.”

132:13 Kut 15:17; Za 48:1, 2; 68:16; 1Fal 18:13Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni,

amepaonea shauku pawe maskani yake:

132:14 Za 80:1; 68:16; 2Sam 6:2“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele;

hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku:

132:15 Za 107:9; 147:14Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele:

nitashibisha maskini wake kwa chakula.

132:16 2Nya 6:41; Ay 8:21; Za 149:5Nitawavika makuhani wake wokovu,

nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha.

132:17 1Sam 2:10; Za 18:28; 84:9; 92:10; Eze 29:21; Lk 1:69; 1Fal 11:36; 2Fal 8:19; 2Nya 21:7“Hapa nitamchipushia Daudi pembe,132:17 Pembe inawakilisha nguvu.

na kuweka taa kwa ajili ya masiya132:17 Masiya yaani mpakwa mafuta. wangu.

132:18 Ay 8:22; 2Sam 12:30Adui zake nitawavika aibu,

bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”

Read More of Zaburi 132