Zaburi 126:1-6 NEN

Zaburi 126:1-6

Zaburi 126

Kurejezwa Kutoka Utumwani

Wimbo wa kwenda juu.

126:1 Ezr 1:1-3; Za 85:1; Hos 6:11; Mdo 12:9Bwana alipowarejeza mateka Sayuni,

tulikuwa kama watu walioota ndoto.

126:2 Mwa 21:6; Ay 8:21; Kum 10:21; Za 65:8; 71:19; Lk 1:49Vinywa vyetu vilijaa kicheko,

ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe.

Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa,

Bwana amewatendea mambo makuu.”

126:3 Za 9:2; 16:11; 106:21; Yoe 2:21, 26Bwana ametutendea mambo makuu,

nasi tumejaa furaha.

126:4 Kum 30:3; Za 107:35; Isa 43:19; 51:3Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa,

kama vijito katika Negebu.

126:5 Za 16:11; 20:5; 23:6; 6:6; 80:5; Yer 50:4; Gal 6:9; Isa 12:1-3; 35:10; 51:11; 60:15; 61:7; Yer 31:6-7, 12Wapandao kwa machozi

watavuna kwa nyimbo za shangwe.

Yeye azichukuaye mbegu zake

kwenda kupanda, huku akilia,

atarudi kwa nyimbo za shangwe,

akichukua miganda ya mavuno yake.

Read More of Zaburi 126