Zaburi 123:1-4 NEN

Zaburi 123:1-4

Zaburi 123

Kuomba Rehema

Wimbo wa kwenda juu.

123:1 Za 68:5; Isa 6:1; 63:15Ninayainua macho yangu kwako,

kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni.

123:2 Za 25:15Kama vile macho ya watumwa

yatazamavyo mkono wa bwana wao,

kama vile macho ya mtumishi wa kike

yatazamavyo mkono wa bibi yake,

ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu,

mpaka atakapotuhurumia.

Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu,

kwa maana tumevumilia dharau nyingi.

Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi,

dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.

Read More of Zaburi 123