Zaburi 121:1-8 NEN

Zaburi 121:1-8

Zaburi 121

Bwana Mlinzi Wetu

Wimbo wa kwenda juu.

Nayainua macho yangu nitazame vilima,

msaada wangu utatoka wapi?

121:2 Mwa 1:1; Za 104:5Msaada wangu hutoka kwa Bwana,

Muumba wa mbingu na dunia.

121:3 1Sam 2:9; Isa 27:3Hatauacha mguu wako uteleze,

yeye akulindaye hatasinzia,

121:4 Za 127:1hakika, yeye alindaye Israeli

hatasinzia wala hatalala usingizi.

121:5 Za 1:6Bwana anakulinda,

Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,

121:6 Isa 49:10jua halitakudhuru mchana,

wala mwezi wakati wa usiku.

121:7 Za 9:9, 10; 91:9, 10; Ay 5:19; Mit 12:21Bwana atakukinga na madhara yote,

atayalinda maisha yako,

121:8 Kum 28:6; Mit 2:8Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka,

tangu sasa na hata milele.

Read More of Zaburi 121