Zaburi 120:1-7 NEN

Zaburi 120:1-7

Zaburi 120

Kuomba Msaada

Wimbo wa kwenda juu.

120:1 2Sam 22:7; Za 18:1; 118:5Katika dhiki yangu namwita Bwana,

naye hunijibu.

120:2 Za 31:18; 52:4Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo

na ndimi za udanganyifu.

Atakufanyia nini,

au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?

120:4 Kum 32:23Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,

kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.

120:5 Mwa 25:13; 2:10; Yer 2:10; 49:28; 1Sam 25:1Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,

kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!

Nimeishi muda mrefu mno

miongoni mwa wale wanaochukia amani.

Mimi ni mtu wa amani;

lakini ninaposema, wao wanataka vita.

Read More of Zaburi 120