Zaburi 119:89-96 NEN

Zaburi 119:89-96

Imani Katika Sheria Ya Bwana

119:89 Za 119:111, 144; 111:8; Isa 51:6; Mt 5:18; 1Pet 1:25Ee Bwana, neno lako ni la milele,

linasimama imara mbinguni.

119:90 Za 36:5; 45:17; 148:6; Ay 8:19Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote,

umeiumba dunia, nayo inadumu.

119:91 Yer 33:25; 31:35; Za 148:6; 104:2-4; Mwa 8:22Sheria zako zinadumu hadi leo,

kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.

119:92 Za 37:4, 5; 112:1; 119:50, 67; Rum 15:4Kama nisingefurahia sheria yako,

ningeangamia katika taabu zangu.

119:93 Za 119:83; 103:5Sitasahau mausia yako kamwe,

kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.

119:94 Za 119:45, 146; 54:1; 116:4; Yer 17:14; 31:18; 42:11; Hos 2:7, 16Uniokoe, kwa maana mimi ni wako,

kwa kuwa nimetafuta mausia yako.

119:95 Za 69:4; 119:99Waovu wanangojea kuniangamiza,

bali mimi ninatafakari sheria zako.

119:96 Za 19:7; Isa 40:8; Mt 5:18Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo,

lakini amri zako hazina mpaka.

Read More of Zaburi 119