Zaburi 119:73-80 NEN

Zaburi 119:73-80

Haki Ya Sheria Ya Bwana

119:73 Mwa 1:27; Ay 4:17; 10:8; Za 139:13-16; 100:3; 138:8Mikono yako ilinifanya na kuniumba,

nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.

119:74 Za 34:2; 119:9; 130:5Wakuchao wafurahie wanaponiona,

kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.

119:75 Za 89:30, 31; 119:7, 138, 172; Ebr 12:5-11Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki,

katika uaminifu wako umeniadhibu.

119:76 Za 6:4; 119:41Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu,

sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

Huruma yako na inijie ili nipate kuishi,

kwa kuwa naifurahia sheria yako.

119:78 Za 119:51; 35:19; 119:86, 161; 25:3; Yer 50:32Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu,

lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.

119:79 Za 119:27, 125Wale wakuchao na wanigeukie mimi,

hao ambao wanazielewa sheria zako.

119:80 Za 119:1; 119:6; 1Fal 8:61; Mwa 26:5Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako,

ili nisiaibishwe.

Read More of Zaburi 119