Zaburi 119:65-72 NEN

Zaburi 119:65-72

Thamani Ya Sheria Ya Bwana

119:65 Isa 50:2; 59:1; Za 119:9, 17; 125:4; Mik 2:7Mtendee wema mtumishi wako

Ee Bwana, sawasawa na neno lako.

119:66 Za 51:6Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri,

kwa kuwa ninaamini amri zako.

119:67 Za 116:10; 95:10; 119:17; Ebr 12:11; Yer 8:4; 31:18; Kum 32:15; Ufu 3:19Kabla sijapata shida nilipotea njia,

lakini sasa ninalitii neno lako.

119:68 Za 100:5; 106:1; 107:1; 135:3; Kut 18:20; 34:6; Mt 19:17Wewe ni mwema, unalotenda ni jema,

nifundishe maagizo yako.

119:69 Ay 13:4; Za 109:2Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo,

nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.

119:70 Mdo 28:27; Za 17:10; Isa 29:13Mioyo yao ni katili na migumu,

bali mimi napendezwa na sheria yako.

119:71 Za 119:67, 75; Ebr 12:10Ilikuwa vyema mimi kupata shida

ili nipate kujifunza maagizo yako.

119:72 Ay 28:17; Za 19:10; Mt 8:10Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu

kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.

Read More of Zaburi 119