Zaburi 119:57-64 NEN

Zaburi 119:57-64

Kujitolea Katika Sheria Ya Bwana

119:57 Kum 32:9; Yer 51:19; Za 119:17, 67, 101; Mao 3:24Ee Bwana, wewe ni fungu langu,

nimeahidi kuyatii maneno yako.

119:58 Kum 4:29; Ezr 9:8; 1Nya 16:11; Za 34:4; 119:41; Mwa 43:29Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote,

nihurumie sawasawa na ahadi yako.

119:59 Yoe 2:13; Lk 15:17; Yos 24:14, 15Nimezifikiri njia zangu

na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.

119:60 Za 119:115Nitafanya haraka bila kuchelewa

kuzitii amri zako.

119:61 Za 119:83, 109, 153, 176Hata waovu wanifunge kwa kamba,

sitasahau sheria yako.

119:62 Za 119:55; 119:7; Mdo 16:25Usiku wa manane ninaamka kukushukuru

kwa sababu ya sheria zako za haki.

119:63 Za 15:4; 101:6, 7; 103:11; 119:56; 111:10Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao,

kwa wote wanaofuata mausia yako.

119:64 Za 33:5; 119:12, 108Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako,

nifundishe maagizo yako.

Read More of Zaburi 119