Zaburi 119:49-56 NEN

Zaburi 119:49-56

Matumaini Katika Sheria Ya Bwana

119:49 Za 119:9, 43Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako,

kwa sababu umenipa tumaini.

119:50 Za 119:25; 27:13; Yer 15:16; Rum 5:3-5; Ebr 6:17-19Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:

Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.

119:51 Za 119:21; Ay 16:10; 17:2; 23:11; Yer 20:7Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka,

hata hivyo sitaiacha sheria yako.

119:52 Za 103:18Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani,

nazo zinanifariji.

119:53 Kut 32:19; 33:4; Za 89:30; Ezr 9:3Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu,

ambao wameacha sheria yako.

119:54 Za 119:172; 101:1; 138:5Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu

popote ninapoishi.

119:55 Za 119:44, 62, 72; 1:2; 42:8; 63:6; 77:2; Isa 26:9; Mdo 16:25Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako,

nami nitatii sheria yako.

119:56 Za 119:4, 100, 134; Hes 15:40Hili limekuwa zoezi langu:

nami ninayatii mausia yako.

Read More of Zaburi 119