Zaburi 119:41-48 NEN

Zaburi 119:41-48

Kuitumainia Sheria Ya Bwana

119:41 Za 6:4; 119:76, 116, 154, 170Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie,

wokovu wako sawasawa na ahadi yako,

119:42 Mit 27:11; Za 42:10ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki,

kwa kuwa ninalitumainia neno lako.

119:43 Za 119:74, 81, 114, 147; 1Fal 17:24Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu,

kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.

119:44 Za 119:33, 34, 55; Kum 6:25Nitaitii amri yako daima,

naam, milele na milele.

119:45 Za 119:94, 155; Yn 8:32, 36; Rum 8:2Nitatembea nikiwa huru,

kwa kuwa nimejifunza mausia yako.

119:46 Mt 10:18; Mdo 26:1, 2; Za 119:6Nitasema sheria zako mbele za wafalme

wala sitaaibishwa,

119:47 Za 119:77, 97, 127, 143, 159, 163, 165kwa kuwa ninazifurahia amri zako

kwa sababu ninazipenda.

119:48 Mwa 24:63Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu,

nami ninatafakari juu ya maagizo yako.

Read More of Zaburi 119