Zaburi 119:33-40 NEN

Zaburi 119:33-40

Maombi Ili Kupata Ufahamu Wa Sheria

119:33 Za 119:12Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako,

nami nitayashika mpaka mwisho.

119:34 Za 119:27, 69, 73, 144, 169; Mit 2:6; Ay 32:8; Yak 1:5; Kum 6:25; Dan 2:21Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako

na kuitii kwa moyo wangu wote.

119:35 Za 119:32; 1:2; 25:4, 5Niongoze kwenye njia ya amri zako,

kwa kuwa huko napata furaha.

119:36 Yos 24:23; Ebr 13:5; Mk 7:21; 12:15; Eze 33:31; 1Tim 6:10Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako,

na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.

119:37 Za 119:9, 25; 71:20; Ay 31:1Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

119:38 Hes 23:19; 2Sam 7:25Mtimizie mtumishi wako ahadi yako,

ili upate kuogopwa.

119:39 Za 119:22; 69:9; 89:51; Isa 25:8; 51:7; 54:4Niondolee aibu ninayoiogopa,

kwa kuwa sheria zako ni njema.

119:40 Za 119:20, 25, 149, 154Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako!

Hifadhi maisha yangu katika haki yako.

Read More of Zaburi 119