Zaburi 119:25-32 NEN

Zaburi 119:25-32

Kuamua Kuitii Sheria Ya Bwana

119:25 Za 44:25; 143:11; 119:9, 50, 107Nimelazwa chini mavumbini,

yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

119:26 Za 25:4; 27:11; 86:11; 1Fal 8:36Nilikueleza njia zangu ukanijibu,

nifundishe sheria zako.

119:27 Za 105:2; 145:5Nijulishe mafundisho ya mausia yako,

nami nitatafakari maajabu yako.

119:28 Za 119:9; 116:3; 18:1; 6:7; Yer 45:3; Isa 51:11; 40:29; 41:10Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni,

uniimarishe sawasawa na neno lako.

119:29 Za 26:4; Hes 6:25; Mit 30:8; Ebr 8:10Niepushe na njia za udanganyifu,

kwa neema unifundishe sheria zako.

119:30 Yos 24:22; Za 26:3; 108:1Nimechagua njia ya kweli,

nimekaza moyo wangu katika sheria zako.

119:31 Kum 10:20Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana,

usiniache niaibishwe.

119:32 1Fal 4:29; Isa 60:5; 2Kor 6:11Nakimbilia katika njia ya maagizo yako,

kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.

Read More of Zaburi 119