Zaburi 119:17-24 NEN

Zaburi 119:17-24

Furaha Katika Sheria Ya Bwana

119:17 Za 13:6; 116:7; 119:67; 103:20Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi;

nitalitii neno lako.

Yafungue macho yangu nipate kuona

mambo ya ajabu katika sheria yako.

119:19 Mwa 23:4; Ebr 11:13Mimi ni mgeni duniani,

usinifiche amri zako.

119:20 Za 84:2; 119:131; 42:2; 63:1; Isa 26:9Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa

juu ya sheria zako wakati wote.

119:21 Za 119:10, 51; 5:5; Ay 30:1; Yer 20:7; 50:32; Kum 27:26; Dan 4:37; Mal 3:15Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa

waendao mbali na amri zako.

119:22 Za 39:8; 119:2Niondolee dharau na dhihaka,

kwa kuwa ninazishika sheria zako.

Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia,

mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako.

Sheria zako ni furaha yangu,

nazo ni washauri wangu.

Read More of Zaburi 119