Zaburi 119:161-168 NEN

Zaburi 119:161-168

Kujiweka Wakfu Kwa Sheria Ya Bwana

119:161 Za 119:23, 122, 157; 119:120; 1Sam 24:14-15Watawala wamenitesa bila sababu,

lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.

119:162 Za 119:25; 41:2Nafurahia ahadi zako

kama mtu aliyepata mateka mengi.

Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo,

lakini napenda sheria yako.

119:164 Za 119:111; 1Sam 30:16; Isa 9:3; 53:12Ninakusifu mara saba kwa siku,

kwa ajili ya sheria zako za haki.

119:165 Za 119:11; 37:11; 37:24; Isa 26:3, 12; 27:5; 32:17; 57:19; 66:12; 1Yn 2:10; Mit 3:2Wanaopenda sheria yako wana amani tele,

wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza.

119:166 Za 119:81Ee Bwana, ninangojea wokovu wako,

nami ninafuata amri zako,

119:167 Za 119:47Ninazitii sheria zako,

kwa sababu ninazipenda mno.

119:168 Za 139:3; Ay 10:4; 23:10; Mit 5:21Nimetii mausia yako na sheria zako,

kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako.

Read More of Zaburi 119