Zaburi 119:153-160 NEN

Zaburi 119:153-160

Maombi Kwa Ajili Ya Msaada

119:153 Za 13:3; 3:7; 44:17; Mao 5:1Yaangalie mateso yangu, uniokoe,

kwa kuwa sijasahau sheria yako.

119:154 Za 119:24, 41; 35:1; 1Sam 24:15; Yer 50:34; Mik 7:9Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako.

119:155 Za 119:94, 118; Ay 5:4Wokovu uko mbali na waovu,

kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.

119:156 Neh 9:27; Yak 5:11; Za 119:25, 149Ee Bwana, huruma zako ni kuu,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako.

119:157 Za 7:1; 44:18Adui wanaonitesa ni wengi,

lakini mimi sitaziacha sheria zako.

119:158 Za 119:104, 136; Kut 32:19Ninawatazama wasioamini kwa chuki,

kwa kuwa hawalitii neno lako.

119:159 Za 119:25; 41:2Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako;

Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.

119:160 Za 119:89; 111:8Maneno yako yote ni kweli,

sheria zako zote za haki ni za milele.

Read More of Zaburi 119