Zaburi 119:145-152 NEN

Zaburi 119:145-152

Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa

119:145 Za 119:10, 22, 55Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote,

nami nitayatii maagizo yako.

119:146 Za 119:94Ninakuita; niokoe

nami nitazishika sheria zako.

119:147 Za 3:3; 57:8; 108:2Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada;

nimeweka tumaini langu katika neno lako.

119:148 Za 63:6; 63:1, 6Sikufumba macho yangu usiku kucha,

ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.

119:149 Za 27:7; 124; 119:40Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako,

Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.

119:150 Za 37:7Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami,

lakini wako mbali na sheria yako.

119:151 Flp 4:5; Za 34:18; 119:142; 145:18Ee Bwana, hata hivyo wewe u karibu,

na amri zako zote ni za kweli.

119:152 Za 119:7, 73, 89; 111:8; Lk 21:33Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako

kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.

Read More of Zaburi 119