Zaburi 119:129-136 NEN

Zaburi 119:129-136

Shauku Ya Kuitii Sheria Ya Bwana

119:129 Za 119:18, 22, 88Sheria zako ni za ajabu,

hivyo ninazitii.

119:130 Za 119:105; 19:7, 10; Mit 1:4; 2Pet 1:19Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,

kunampa mjinga ufahamu.

119:131 Za 42:1; 119:20Nimefungua kinywa changu na kuhema,

nikitamani amri zako.

119:132 2Sam 24:14; Kut 4:31; Za 6:4; 9:13; 5:11; 106:4; 1Sam 1:11Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote

wale wanaolipenda jina lako.

119:133 Kum 6:12; Za 119:9, 11, 122; Rum 6:16Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako,

usiache dhambi yoyote initawale.

119:134 Lk 1:74; Za 119:56, 88, 122Niokoe na uonevu wa wanadamu,

ili niweze kutii mausia yako.

119:135 Hes 6:25; Za 4:6; 80:3; 4:6; 119:12Mwangazie mtumishi wako uso wako

na unifundishe amri zako.

119:136 Yer 9:1; 9:1, 18; 13:17; 14:17; Mao 1:16; 3:48; Isa 22:4; 42:24; Eze 9:4; Za 6:6; 119:158; 106:25Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu,

kwa kuwa sheria yako haifuatwi.

Read More of Zaburi 119