Zaburi 119:113-120 NEN

Zaburi 119:113-120

Usalama Ndani Ya Sheria Ya Bwana

119:113 1Fal 18:21; Yak 1:8; 4:8; Za 119:47Ninachukia watu wa nia mbili,

lakini ninapenda sheria yako.

119:114 Za 18:2; 119:43; 32:7; Mwa 15:1Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu,

nimeweka tumaini langu katika neno lako.

119:115 Za 6:8; Mt 7:23Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya,

ili niweze kushika amri za Mungu wangu!

119:116 Za 18:35; 41:3; 55:22; 119:41; Isa 46:4; Rum 5:5; 9:33Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi;

usiache matumaini yangu yakavunjwa.

119:117 Isa 41:10; 46:4; Za 34:4; 119:6; 71:6; Yn 10:28; Rum 14:4Nitegemeze, nami nitaokolewa,

nami daima nitayaheshimu maagizo yako.

119:118 Za 119:10Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako,

kwa maana udanganyifu wao ni bure.

119:119 Isa 1:22, 25; Eze 18:19; Za 119:47Waovu wa nchi unawatupa kama takataka,

kwa hivyo nazipenda sheria zako.

119:120 Ay 4:14Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe,

ninaziogopa sheria zako.

Read More of Zaburi 119