Zaburi 119:1-8 NEN

Zaburi 119:1-8

Zaburi 119119:0 Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi 22 za alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T).

Sifa Za Sheria Ya Bwana

Kujifunza Sheria Ya Bwana

119:1 Mwa 17:1; Za 1:2; 128:1; Kum 18:13; Mit 11:20Heri wale walio waadilifu katika njia zao,

wanaoenenda katika sheria ya Bwana.

119:2 Za 40:16; 112:1; 119:146; Isa 56:2; Kum 10:12; Mit 9:7; 1Nya 16:11Heri wale wanaozishika shuhuda zake,

wamtafutao kwa moyo wao wote.

119:3 Za 59:4; 128:1; Yn 3:9; 5:18; Yer 6:16; 7:23; Rum 7:16, 17Wasiofanya lolote lililo baya,

wanaoenenda katika njia zake.

119:4 Za 103:18; 119:56; Kum 6:17Umetoa maagizo yako

ili tuyatii kwa ukamilifu.

119:5 Law 19:37; Yer 31:33; 2Kor 3:5; Rum 7:22, 23Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara

katika kuyatii maagizo yako!

119:6 Za 119:46, 80, 117; Ay 22:26; 1Yn 2:28Hivyo mimi sitaaibishwa

ninapozingatia amri zako zote.

119:7 Kum 4:8119:7 Za 90:13; 103:13; 119:47Nitakusifu kwa moyo mnyofu

ninapojifunza sheria zako za haki.

119:8 Za 38:21Nitayatii maagizo yako;

usiniache kabisa.

Read More of Zaburi 119