Zaburi 118:17-29 NEN

Zaburi 118:17-29

118:17 Hab 1:12; Za 6:5; 64:9; 71:16; 73:28; Kum 32:3Sitakufa, bali nitaishi,

nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda.

118:18 Yer 31:18; Ebr 12:5; 1Kor 11:32; Za 86:13; Mit 3:11, 12Bwana ameniadhibu vikali,

lakini hakuniacha nife.

118:19 Isa 26:2; Za 24:7; 100:4Nifungulie malango ya haki,

nami nitaingia na kumshukuru Bwana.

118:20 Ufu 22:14; Za 122:1, 2; 15:1, 2; 24:3-4Hili ni lango la Bwana

ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.

118:21 Za 118:5; 27:1Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu,

umekuwa wokovu wangu.

118:22 Mdo 4:11; Isa 8:14; 17:10; 19:13; 28:16; Mt 21:42; Lk 20:17; Zek 4:7; 10:4; Mk 12:10; 1Pet 2:7; Efe 2:20Jiwe walilolikataa waashi,

limekuwa jiwe kuu la pembeni.

118:23 Ay 5:9; Mt 21:42; Mk 12:11Bwana ametenda hili,

nalo ni la kushangaza machoni petu.

118:24 Za 70:4; 2Kor 6:2Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,

tushangilie na kufurahi ndani yake.

118:25 Za 28:9; 116:4Ee Bwana, tuokoe,

Ee Bwana, utujalie mafanikio.

118:26 Zek 4:7; Mt 11:3; 21:9; 23:39; Mk 11:9; Lk 13:35; 19:38; Yn 12:13; Za 129:8Heri yule ajaye kwa jina la Bwana.

Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki.

118:27 Za 27:1; Mal 4:2; Isa 60:1; 58:10; 19:20; 1Fal 18:21; 1Pet 2:9; Mik 7:9; Law 23:40; Es 8:2; Kut 27:2Bwana ndiye Mungu,

naye ametuangazia nuru yake.

Mkiwa na matawi mkononi,

unganeni kwenye maandamano ya sikukuu

hadi kwenye pembe za madhabahu.

118:28 Mwa 28:21; Za 16:2; 63:1; Isa 25:1; Kut 15:2Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru,

wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

Read More of Zaburi 118