Zaburi 118:1-16 NEN

Zaburi 118:1-16

Zaburi 118

Shukrani Kwa Ajili Ya Ushindi

118:1 1Nya 16:8; Ezr 3:11; 2Nya 7:3; 5:13Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

118:2 Za 115:9; 106:1; 136:1-26Israeli na aseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

118:3 Kut 30:30; Za 115:10Nyumba ya Aroni na iseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

118:4 Za 115:11Wote wamchao Bwana na waseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

118:5 Za 18:6; 31:7; 77:2; 120:1; 118:21; 34:4; 86:7; 116:1; 138:3Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana,

naye akanijibu kwa kuniweka huru.

118:6 Kum 31:6; Ebr 13:5; Za 56:5Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

118:7 Kum 33:29; Ebr 13:6; Za 54:4Bwana yuko pamoja nami,

yeye ni msaidizi wangu.

Nitawatazama adui zangu

wakiwa wameshindwa.

118:8 Yer 17:5, 7; Za 9:9; 62:8; 5:11; 37:3; 40:4; 108:12; Isa 25:4; 57:13; 2:22; 2Nya 32:7-8Ni bora kumkimbilia Bwana

kuliko kumtumainia mwanadamu.

118:9 Za 146:3; Isa 30:2, 3Ni bora kumkimbilia Bwana

kuliko kuwatumainia wakuu.

118:10 Za 37:9Mataifa yote yalinizunguka,

lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

118:11 Za 88:17; 3:6Walinizunguka pande zote,

lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

118:12 Mhu 7:6; Za 58:9; 37:9; Kum 1:44Walinizunguka kama kundi la nyuki,

lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo;

kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.

118:13 Za 118:7; 86:17; 2Nya 18:31Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka,

lakini Bwana alinisaidia.

118:14 Kut 15:2; Za 62:2Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu,

yeye amefanyika wokovu wangu.

118:15 Ay 8:21; Lk 1:51; Za 106:5; 89:13; 108:6; Kut 15:6Sauti za shangwe na ushindi

zinavuma hemani mwa wenye haki:

“Mkono wa kuume wa Bwana

umetenda mambo makuu!

118:16 Kut 15:6Mkono wa kuume wa Bwana

umeinuliwa juu,

mkono wa kuume wa Bwana

umetenda mambo makuu!”

Read More of Zaburi 118