Zaburi 116:12-19 NEN

Zaburi 116:12-19

116:12 Za 103:2; 106:1Nimrudishie Bwana nini

kwa wema wake wote alionitendea?

116:13 Za 105:1Nitakiinua kikombe cha wokovu

na kulitangaza jina la Bwana.

116:14 Hes 30:2; Za 66:13Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana

mbele za watu wake wote.

116:15 Za 72:14; Hes 23:10; Ay 5:26; Lk 16:22; Ufu 14:13Kifo cha watakatifu kina thamani

machoni pa Bwana.

116:16 Za 119:125; 143:12; 86:16; Ay 12:18Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,

mimi ni mtumishi wako,

mwana wa mjakazi wako;116:16 Au: mwanao mwaminifu.

umeniweka huru

toka katika minyororo yangu.

116:17 Law 7:12; Ezr 1:4Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru

na kuliita jina la Bwana.

116:18 Za 116:14; Law 22:18Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana

mbele za watu wake wote,

116:19 Za 102:21; 92:13; 135:2; 96:8; 100:4katika nyua za nyumba ya Bwana,

katikati yako, ee Yerusalemu.

Msifuni Bwana.

Read More of Zaburi 116