Zaburi 116:1-11 NEN

Zaburi 116:1-11

Zaburi 116

Shukrani Kwa Kuokolewa Kutoka Mauti

116:1 Za 18:1; 31:22; 40:1; 6:9; 28:2Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu;

amesikia kilio changu ili anihurumie.

116:2 Za 5:1Kwa sababu amenitegea sikio lake,

nitamwita siku zote za maisha yangu.

116:3 2Sam 22:6; Za 18:4-5Kamba za mauti zilinizunguka,

maumivu makuu ya kuzimu yalinipata,

nikalemewa na taabu na huzuni.

116:4 Za 80:2, 18; 118:5Ndipo nikaliitia jina la Bwana:

“Ee Bwana, niokoe!”

116:5 Kut 22:27; 9:27; Ezr 9:15; Za 11:7; 86:15; 2Nya 12:6; Neh 9:8; Yer 12:1; Mao 1:18; Ufu 16:5Bwana ni mwenye neema na haki,

Mungu wetu ni mwingi wa huruma.

116:6 Za 79:8; 18:3; 22:5; 107:13Bwana huwalinda wanyenyekevu,

nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.

116:7 Za 13:6; 106:1; 142:7; 46:10; 62:1; 131:2; Mt 11:29; Yer 6:16Ee nafsi yangu, tulia tena,

kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako.

116:8 Za 86:13Kwa kuwa wewe, Ee Bwana,

umeniokoa nafsi yangu na mauti,

macho yangu kutokana na machozi,

miguu yangu kutokana na kujikwaa,

116:9 Mwa 5:22; Za 56:13; 89:15; 27:13; Ay 28:13; Isa 38:11; Yer 11:9ili niweze kutembea mbele za Bwana,

katika nchi ya walio hai.

116:10 Za 9:18; 72:2; 107:17; 119:67, 71, 75; 2Kor 4:13Niliamini, kwa hiyo nilisema,

“Mimi nimeteseka sana.”

116:11 Yer 9:3-5Katika taabu yangu nilisema,

“Wanadamu wote ni waongo.”

Read More of Zaburi 116