Zaburi 115:1-11
Zaburi 115
Mungu Mmoja Wa Kweli
115:1 Za 29:2; 96:8; Kut 34:6Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi,
bali utukufu ni kwa jina lako,
kwa sababu ya upendo
na uaminifu wako.
115:2 Za 42:3, 10; 79:10; Yoe 2:17Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wao?”
115:3 Ezr 5:11; Neh 1:4; Za 136:26; 135:6; 103:19; Mit 6:9; Dan 4:35; 1Nya 16:26Mungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lolote limpendezalo.
115:4 2Fal 19:18; 2Nya 32:19; Yer 10:3-5; Mdo 19:26; Kum 4:28; Ufu 9:20; Za 135:15, 16; Isa 40:19; Hos 8:6; 1Kor 10:19, 20Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
115:5 Yer 10:5Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
115:8 Za 135:18; Isa 44:9, 10; Yon 2:8; Hab 2:18Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
115:9 Za 37:3; 62:8; 33:20; Mit 30:5Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
115:10 Kut 30:30; Za 118:3; Mal 2:7Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
115:11 Za 22:23; 103:11; 118:4Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.