Zaburi 113:1-9 NEN

Zaburi 113:1-9

Zaburi 113

Kumsifu Bwana Kwa Wema Wake

113:1 Za 22:23; 34:22; 103:21; 134:1Msifuni Bwana.

Enyi watumishi wa Bwana msifuni,

lisifuni jina la Bwana.

113:2 Za 30:4; 48:10; 145:21; 148:13; 149:3; 115:18; 131:3; Isa 12:4; Dan 2:20Jina la Bwana na lisifiwe,

sasa na hata milele.

113:3 Isa 24:15; 45:6; 59:19; Mal 1:11Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,

jina la Bwana linapaswa kusifiwa.

113:4 Za 99:2; 8:1; 57:11Bwana ametukuka juu ya mataifa yote,

utukufu wake juu ya mbingu.

113:5 Kut 8:10; Ay 16:19; Za 35:10; 103:19Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu,

Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,

113:6 Za 11:4; 138:6; Isa 57:15ambaye huinama atazame chini

aone mbingu na nchi?

113:7 1Sam 2:8; Za 35:10; 68:10; 140:12; 107:41Huwainua maskini kutoka mavumbini,

na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,

113:8 2Sam 9:11huwaketisha pamoja na wakuu,

pamoja na wakuu wa watu wake.

113:9 1Sam 2:5Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,

akiwa mama watoto mwenye furaha.

Msifuni Bwana.

Read More of Zaburi 113