Zaburi 109:21-31 NEN

Zaburi 109:21-31

109:21 Kut 9:16; Za 3:7; 23:3; 69:16Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi,

unitendee wema kwa ajili ya jina lako,

uniokoe kwa wema wa pendo lako.

Maana mimi ni maskini na mhitaji,

moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.

109:23 Ay 14:2Ninafifia kama kivuli cha jioni,

nimerushwa-rushwa kama nzige.

109:24 Ebr 12:12; Ay 16:8; Za 35:13Magoti yangu yamelegea kwa kufunga,

mwili wangu umedhoofika na kukonda.

109:25 Za 22:6; Ay 16:4; Mt 27:39; Mk 15:29; Isa 37:22Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu,

wanionapo, hutikisa vichwa vyao.

109:26 Za 12:1; 119:86Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie,

niokoe sawasawa na upendo wako.

109:27 Ay 37:7Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako,

kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili.

109:28 2Sam 16:12; Za 66:4; Isa 35:10; 51:11; 54:1; 65:14; Hes 22:12Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki,

watakaposhambulia wataaibishwa,

lakini mtumishi wako atashangilia.

109:29 Za 35:26Washtaki wangu watavikwa fedheha,

na kufunikwa na aibu kama joho.

109:30 Za 35:18Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana,

katika umati mkubwa nitamsifu.

109:31 Za 16:8; 108:6Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji,

kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu.

Read More of Zaburi 109