Zaburi 109:1-20 NEN

Zaburi 109:1-20

Zaburi 109

Lalamiko La Mtu Aliyeko Kwenye Shida

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

109:1 Kut 15:2; Yer 17:14; Ay 34:29; Za 83:1Ee Mungu, ambaye ninakusifu,

usiwe kimya,

109:2 Za 43:1; 52:4kwa maana watu waovu na wadanganyifu

wamefungua vinywa vyao dhidi yangu;

wasema dhidi yangu

kwa ndimi za udanganyifu.

109:3 Za 69:4; 35:7; 35:7, 10; Yn 15:25; 1Sam 19:4, 5Wamenizunguka kwa maneno ya chuki,

wananishambulia bila sababu.

109:4 Za 69:13; 141:5Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki,

lakini mimi ninawaombea.

109:5 Mwa 44:4; Za 38:20Wananilipiza mabaya kwa mema,

chuki badala ya urafiki wangu.

109:6 1Nya 21:1; Ay 1:6; Zek 3:1Agiza mtu mwovu ampinge,

mshtaki109:6 Mshtaki hapa maana yake ni Shetani. asimame mkono wake wa kuume.

109:7 Za 1:5; Mit 28:9; Zek 3:1Anapohukumiwa, apatikane na hatia,

nayo maombi yake yamhukumu.

109:8 Ay 15:32; Mdo 1:20Siku zake za kuishi na ziwe chache,

nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine.

109:9 Kut 22:24; Yer 18:21Watoto wake na waachwe yatima,

mke wake na awe mjane.

109:10 Mwa 4:12Watoto wake na watangetange wakiomba,

na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao.

109:11 Hes 14:3; Isa 1:7; 6:11; 36:1; Mao 5:2; Neh 5:3; Ay 20:18; 18:9Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo,

matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni.

109:12 Ay 5:4Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema

wala wa kuwahurumia yatima wake.

109:13 Za 21:10; 9:5; 37:28; Hes 14:12; Mit 10:7; Ay 18:19Uzao wake na ukatiliwe mbali,

majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.

109:14 Kut 20:5Maovu ya baba zake na yakumbukwe

mbele za Bwana,

dhambi ya mama yake

isifutwe kamwe.

109:15 Za 90:8; Kut 17:14; Kum 32:26; Ay 18:17Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana,

ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.

109:16 Ay 20:19; Za 35:10; 34:18Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema,

bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,

aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.

109:17 Mit 28:27; Mt 7:2Alipenda kulaani,

nayo laana ikampata;

hakupenda kubariki,

kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.

109:18 Za 10:7; Hes 5:22Alivaa kulaani kama vazi lake,

nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji,

kwenye mifupa yake kama mafuta.

109:19 Za 109:29; 73:6; Eze 7:27Na iwe kama joho alilozungushiwa,

kama mshipi aliofungiwa daima.

109:20 Kut 32:34; Za 54:5; 94:23; 7:10; Isa 3:11; 2Tim 4:14Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu,

kwa wale wanaoninenea mabaya.

Read More of Zaburi 109