Zaburi 108:6-13 NEN

Zaburi 108:6-13

108:6 Ay 40:14Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,

ili wale uwapendao wapate kuokolewa.

108:7 Za 89:35; 68:35; 102:19; Mwa 12:6; 33:17Mungu amenena kutoka patakatifu pake:

“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi

na kulipima Bonde la Sukothi.

108:8 Za 78:68; Mwa 49:10Gileadi ni yangu, Manase ni yangu,

Efraimu ni kofia yangu ya chuma,

nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.

108:9 Mwa 19:37; 2Sam 8:1, 13-14Moabu ni sinia langu la kunawia,

juu ya Edomu natupa kiatu changu;

nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”

108:10 Za 60:9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?

Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?

108:11 Za 44:9Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,

na hutoki tena na majeshi yetu?

108:12 Isa 10:3; 30:3, 5; 31:3; Yer 2:36; 17:7; Za 118:8; 146:3Tuletee msaada dhidi ya adui,

kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.

108:13 Za 44:5; Isa 22:5; 63:3, 6; 25:10; Mao 1:15; Mal 4:3; Ufu 14:9Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,

naye atawaponda adui zetu.

Read More of Zaburi 108