Zaburi 108:1-5 NEN

Zaburi 108:1-5

Zaburi 108

Kuomba Msaada Dhidi Ya Adui

(Zaburi 57:7-11; 60:5-12)

Wimbo. Zaburi ya Daudi.

108:1 Za 112:7; 119:30, 112; 18:49Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti;

nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

108:2 Ay 21:12Amka, kinubi na zeze!

Nitayaamsha mapambazuko.

Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;

nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

108:4 Hes 14:18; Kum 7:9; Kut 34:6; Za 36:5; Mik 7:18-20Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu;

uaminifu wako unazifikia anga.

108:5 Za 8:1; 57:5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,

utukufu wako na uenee duniani kote.

Read More of Zaburi 108