Zaburi 107:33-43 NEN

Zaburi 107:33-43

107:33 1Fal 17:1; Yoe 1:20; Isa 41:15; 42:15; 50:2; 34:9, 10; Eze 30:12; Nah 1:4; Za 74:15; 104:10Yeye aligeuza mito kuwa jangwa,

chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu,

107:34 Mwa 13:10nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa,

kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo.

107:35 2Fal 3:17; Za 105:41; 126:4; Isa 43:19; 51:3; 35:7; Ay 38:26Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji,

nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo;

107:36 Mdo 17:26aliwaleta wenye njaa wakaishi humo,

nao wakajenga mji wangeweza kuishi.

107:37 2Fal 19:29; Isa 37:30Walilima mashamba na kupanda mizabibu,

nayo ikazaa matunda mengi,

107:38 Mwa 12:2; 49:25; Kum 7:13Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana,

wala hakuruhusu mifugo yao kupungua.

107:39 2Fal 10:32; Eze 5:12; Za 44:9Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa

kwa kuonewa, maafa na huzuni.

107:40 Ay 12:18, 21; Kum 32:10Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu,

aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia.

107:41 1Sam 2:8; 2Sam 7:8; Za 113:7-9; Ay 21:11; 8:7Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao,

na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo.

107:42 Ay 22:19; 5:16; Mit 10:11; Rum 3:19; Za 97:10-12Wanyofu wataona na kufurahi,

lakini waovu wote watafunga vinywa vyao.

107:43 Yer 9:12; Hos 14:9; Za 103:11; Dan 12:10Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya,

na atafakari upendo mkuu wa Bwana.

Read More of Zaburi 107