Zaburi 105:37-45
105:37 Kut 3:21, 22Akawatoa Israeli katika nchi
wakiwa na fedha na dhahabu nyingi,
wala hakuna hata mmoja
kutoka kabila zao aliyejikwaa.
105:38 Kut 15:16Misri ilifurahi walipoondoka,
kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia.
105:39 Kut 13:21; 1Kor 10:1; Za 78:14; Neh 9:12Alitandaza wingu kama kifuniko,
na moto kuwamulikia usiku.
105:40 Za 78:18; Kut 16:4; Yn 6:31; Kut 16:12Waliomba, naye akawaletea kware,
akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.
105:41 Hes 20:11; 1Kor 10:4; Kut 17:6; Neh 9:15; Isa 48:21Alipasua mwamba, maji yakabubujika,
yakatiririka jangwani kama mto.
105:42 Mwa 15:1-4, 13-16; 13:14-17Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu,
aliyompa Abrahamu mtumishi wake.
105:43 Kut 15:1-19; Za 106:12Aliwatoa watu wake kwa furaha,
wateule wake kwa kelele za shangwe,
105:44 Kum 6:10-11; Za 106:12akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi
wa mali wengine walikuwa wameitaabikia:
105:45 Kum 6:14-21; 4:1, 40; Za 105:35; 78:5-7alifanya haya ili wayashike mausia yake
na kuzitii sheria zake.
Msifuni Bwana.105:45 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.