Zaburi 105:23-36
105:23 Mdo 7:15; 13:17; Mwa 46:6; 47:28; Za 78:51Kisha Israeli akaingia Misri,
Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu.
105:24 Kut 1:7; Kum 26:7; Mdo 7:17Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana,
akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao,
105:25 Kut 4:21; 1:6-10; Mdo 7:19ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake,
wakatenda hila dhidi ya watumishi wake.
105:26 Kut 3:10; 4:16; Hes 33:1; 16:5; 17:5-8Akamtuma Mose mtumishi wake,
pamoja na Aroni, aliyemchagua.
105:27 Za 105:28-37; Kut 7:8; 12:51; 4:17; 10:1; 3:20; Dan 4:3Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao,
miujiza yake katika nchi ya Hamu.
105:28 Mwa 1:4; Za 99:7; Kut 10:22; 7:22Alituma giza na nchi ikajaa giza,
kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?
105:29 Za 78:44; Kut 7:21Aligeuza maji yao kuwa damu,
ikasababisha samaki wao kufa.
105:30 Kut 8:2, 6Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia
hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.
105:31 Za 78:45; 107:25; 148:8; Kut 8:16-18; 8:21-24Alisema, yakaja makundi ya mainzi,
na viroboto katika nchi yao yote.
105:32 Kut 9:22-25; Ay 38:22; Za 78:47Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe,
yenye umeme wa radi nchini yao yote,
105:33 Za 78:47; Kut 10:5, 12akaharibu mizabibu yao na miti ya tini,
na akaangamiza miti ya nchi yao.
105:34 Za 107:25; Kut 10:4, 12-15; 1Fal 8:27; Yoe 1:6Alisema, nzige wakaja,
tunutu wasio na idadi,
wakala kila jani katika nchi yao,
wakala mazao ya ardhi yao.
105:36 Kut 4:23; 12:12Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao,
matunda ya kwanza ya ujana wao wote.