Zaburi 105:1-11
Zaburi 105
Uaminifu Wa Mungu Kwa Israeli
(1 Nyakati 16:8-22)
105:1 1Nya 16:34; Za 80:18; 99:6; 116:13; Yoe 2:32; Mdo 2:21; Isa 12:4Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
105:2 Za 30:4; 146:2; 33:3; 96:1; 7:17; 18:49; 27:6; 59:17; 71:22; 75:1Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa,
waambieni matendo yake yote ya ajabu.
105:3 Za 89:16Lishangilieni jina lake takatifu,
mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
105:4 Za 24:6; 27:8Mtafuteni Bwana na nguvu zake,
utafuteni uso wake siku zote.
105:5 Za 40:5; Kum 7:18; 8:2Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,
miujiza yake na hukumu alizozitamka,
105:6 Za 105:42; Kum 10:15; Za 106:5enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake,
enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
105:7 Isa 26:8Yeye ndiye Bwana Mungu wetu,
hukumu zake zimo duniani pote.
105:8 Mwa 9:15; Za 106:45; 111:5; Eze 16:60; Lk 1:72Hulikumbuka agano lake milele,
neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
105:9 Mwa 22:16-18; 15:18; Ebr 6:17; Lk 1:73; 17:2; 12:7; Gal 3:15-18; Dan 9:4agano alilolifanya na Abrahamu,
kiapo alichomwapia Isaki.
105:10 Mwa 28:13-15; Isa 55:3Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,
kwa Israeli liwe agano la milele:
105:11 Mwa 12:7; Hes 34:2“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani
kuwa sehemu utakayoirithi.”