Zaburi 104:31-35 NEN

Zaburi 104:31-35

104:31 Kut 40:35; Rum 11:36; Mwa 1:4; Za 8:1Utukufu wa Bwana na udumu milele,

Bwana na azifurahie kazi zake:

104:32 Kut 19:18; Hab 3:10; Za 97:4; 144:5yeye aitazamaye dunia, nayo ikatetemeka,

aigusaye milima, nayo ikatoa moshi.

104:33 Kut 15:1; Za 108:1Nitamwimbia Bwana maisha yangu yote;

nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.

104:34 Za 2:11; 9:2; 32:11Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye,

ninapofurahi katika Bwana.

104:35 Ay 7:10; Za 28:6; 37:38; 105:45; 106:48Lakini wenye dhambi na watoweke katika dunia

na waovu wasiwepo tena.

Ee nafsi yangu, msifu Bwana.

Msifuni Bwana.104:35 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.

Read More of Zaburi 104