Zaburi 104:1-18 NEN

Zaburi 104:1-18

Zaburi 104

Kumsifu Muumba

104:1 Za 103:22; Ay 40:10Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana,

umejivika utukufu na enzi.

104:2 Yer 43:12; 51:15; 1Tim 6:16; Ay 9:8; 37:18; Isa 44:24; 49:18, 22; 42:5; 40:22; Zek 12:1; Za 18:12; 19:4Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi,

amezitandaza mbingu kama hema

104:3 Amo 9:6; Za 18:10; 24:2; Kum 33:26; Isa 19:1; Nah 1:3; 2Fal 12:11na kuziweka nguzo za orofa yake juu ya maji.

Huyafanya mawingu kuwa gari lake,

na hupanda kwenye mbawa za upepo.

104:4 Za 148:8; Mwa 3:24; 2Fal 2:11; Ebr 1:7Huzifanya pepo kuwa wajumbe104:4 Au: malaika. wake,

miali ya moto watumishi wake.

104:5 Kut 31:17; Ay 26:7; Za 24:1, 2; 121:2; 102:25; 1Sam 2:8Ameiweka dunia kwenye misingi yake,

haiwezi kamwe kuondoshwa.

104:6 Mwa 7:19; 1:2; 2Pet 3:6Uliifunika kwa kilindi kama kwa vazi,

maji yalisimama juu ya milima.

104:7 Za 18:15; 29:3; Kut 9:23Lakini kwa kukemea kwako maji yalikimbia,

kwa sauti ya radi yako yakatoroka,

104:8 Za 33:7; Ay 38:10yakapanda milima, yakateremka mabondeni,

hadi mahali pale ulipoyakusudia.

104:9 Yer 5:22; Za 16:6; 33:7; Ay 26:10; Mwa 1:9; 9:11Uliyawekea mpaka ambao hayawezi kuuvuka,

kamwe hayataifunika dunia tena.

104:10 Za 107:33; Isa 41:16Huzifanya chemchemi zimwage maji mabondeni,

hutiririka kati ya milima.

104:11 Za 104:13; Mwa 16:12; Isa 32:14; Yer 14:6Huwapa maji wanyama wote wa kondeni,

punda-mwitu huzima kiu yao.

104:12 Za 104:17; Mt 8:20; 13:32Ndege wa angani hufanya viota kando ya maji,

huimba katikati ya matawi.

104:13 Za 135:7; 147:8; Yer 10:13Huinyeshea milima kutoka orofa zake,

dunia inatoshelezwa kwa matunda ya kazi yake.

104:14 Ay 38:27; 28:5; Mwa 1:30; Za 147:8; 136:25Huyafanya majani ya mifugo yaote,

na mimea kwa watu kulima,

wajipatie chakula kutoka ardhini:

104:15 Mwa 14:18; Amu 9:13; Za 23:5; 92:10; Lk 7:46; Kum 8:3; Mit 31:6, 7; Yer 12:12; Mk 14:23; Mhu 10:19; Yn 2:9, 10divai ya kuufurahisha moyo wa mwanadamu,

mafuta kwa ajili ya kungʼarisha uso wake,

na mkate wa kutia mwili nguvu.

104:16 Mwa 1:11; Za 29:5; 72:16; Hes 24:6Miti ya Bwana inanyeshewa vizuri,

mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.

104:17 Za 104:12Humo ndege hufanya viota vyao,

korongo ana nyumba yake kwenye msunobari.

104:18 Mit 30:26; Kum 14:5Milima mirefu ni makao ya mbuzi-mwitu,

majabali ni kimbilio la pelele.

Read More of Zaburi 104