Zaburi 102:1-11
Zaburi 102
Maombi Ya Mtu Mwenye Taabu
Maombi ya mtu aliyechoka. Anapoteseka na kumimina malalamiko yake kwa Bwana.
102:1 Za 4:1; Kut 2:23Ee Bwana, usikie maombi yangu,
kilio changu cha kuomba msaada kikufikie.
102:2 Za 22:24; 31:2; 88:2; 2Fal 19:16Usinifiche uso wako
ninapokuwa katika shida.
Unitegee sikio lako,
ninapoita, unijibu kwa upesi.
Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi,
mifupa yangu inaungua kama kaa la moto.
102:4 Za 37:2; 90:5-6; 1Sam 1:7; Ezr 10:6; Ay 33:26Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani,
ninasahau kula chakula changu.
102:5 Za 6:6Kwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu,
nimebakia ngozi na mifupa.
102:6 Isa 34:11; Sef 2:14; Kum 14:15-17; Ay 30:29Nimekuwa kama bundi wa jangwani,
kama bundi kwenye magofu.
102:7 Za 77:4; 38:11Nilalapo sipati usingizi,
nimekuwa kama ndege mpweke
kwenye paa la nyumba.
102:8 Za 31:11; 42:10; Mdo 23:12Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki,
wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana.
102:9 Isa 44:20; Za 6:6; 42:3; 80:5Ninakula majivu kama chakula changu
na nimechanganya kinywaji changu na machozi
102:10 Za 7:11; 38:3; 30:7kwa sababu ya ghadhabu yako kuu,
kwa maana umeniinua na kunitupa kando.
102:11 1Nya 29:15; Ay 14:2; 8:12; Za 39:6; Yak 1:10Siku zangu ni kama kivuli cha jioni,
ninanyauka kama jani.