Zaburi 10:12-18 NEN

Zaburi 10:12-18

10:12 Za 3:7; 9:12, 13; 17:7; 20:6; 106:26; Isa 26:11; Mik 5:9Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu.

Usiwasahau wanyonge.

10:13 Ay 31:14Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu?

Kwa nini anajiambia mwenyewe,

“Hataniita nitoe hesabu?”

10:14 Za 22:11; 37:5; Kum 33:29Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,

umekubali kuyapokea mkononi mwako.

Mhanga anajisalimisha kwako,

wewe ni msaada wa yatima.

10:15 Ay 31:22Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya,

mwite atoe hesabu ya maovu yake

ambayo yasingejulikana.

10:16 Kut 15:18; Kum 8:20Bwana ni Mfalme milele na milele,

mataifa wataangamia watoke nchini mwake.

10:17 Za 9:12; Kut 22:23Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa,

wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,

10:18 Kum 24:17; Za 146:9; 9:9ukiwatetea yatima na walioonewa,

ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.

Read More of Zaburi 10