Zaburi 10:1-11 NEN

Zaburi 10:1-11

Zaburi 1010 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 9 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.

Sala Kwa Ajili Ya Haki

10:1 Za 13:1; 22:1, 11; 35:22; 38:21; 71:12Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali?

Kwa nini unajificha wakati wa shida?

10:2 Ay 20:19; Mit 5:22; 10:3; Za 49:6; 94:4; Yer 48:30; Ay 1:5Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini,

waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.

Hujivunia tamaa za moyo wake;

humbariki mlafi na kumtukana Bwana.

10:4 Za 12:3-5; 36:1; 2Fal 18:35; Ay 21:15Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu,

katika mawazo yake yote

hakuna nafasi ya Mungu.

10:5 Za 18:27; 105:5; Mit 6:17; Isa 13:11; Yer 48:29Njia zake daima hufanikiwa;

hujivuna na amri zako ziko mbali naye,

huwacheka kwa dharau adui zake wote.

10:6 Ufu 18:7Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa,

daima nitakuwa na furaha,

kamwe sitakuwa na shida.”

10:7 Mhu 4:1; Rum 3:14; Isa 30:12; Ay 20:12; Za 73:8; 119:134Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho;

shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.

10:8 Za 37:32; 59:3; 71:10; Mit 1:11; Yer 5:26; Mik 7:2; Hos 6:9Huvizia karibu na vijiji;

kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia,

akivizia wapitaji.

10:9 Ay 18:8Huvizia kama simba aliye mawindoni;

huvizia kumkamata mnyonge,

huwakamata wanyonge na kuwaburuza

katika wavu wake.

10:10 Ay 9:17Mateka wake hupondwa, huzimia;

wanaanguka katika nguvu zake.

10:11 Ay 22:13; 22:14; Za 42:9; 77:9Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau,

huficha uso wake na haoni kabisa.”

Read More of Zaburi 10