Zaburi 9:1-6
Zaburi 99 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 10 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Haki Yake
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa muth-labeni.9:0 Muth-labeni ni mtajo mmojawapo katika lugha za muziki. Zaburi ya Daudi.
9:1 Za 86:12; 11:1; 119:2, 10; 145:5; 138:1; Kum 4:34Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote,
nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
9:2 Ay 22:19; Isa 25:9; Za 14:7; 31:7; 70:4; 92:1; 97:8; 126:3; Mit 23:15; Yoe 2:21; Ufu 19:7; Yer 30:19; Sef 3:14; Mt 5:12; 2Nya 31:2Nitafurahi na kushangilia ndani yako.
Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.
Adui zangu wamerudi nyuma,
wamejikwaa na kuangamia mbele zako.
9:4 1Fal 8:45; Isa 6:1; Ay 16:21; Za 7:11; 11:4; 47:8; 67:4; 98:9; 1Pet 2:23Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu;
umeketi kwenye kiti chako cha enzi,
ukihukumu kwa haki.
9:5 Mwa 20:7; 37:10; 1Nya 16:21; Za 59:5; 105:14; Isa 26:14; 66:15; Ay 18:17; Kum 9:14Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu;
umeyafuta majina yao milele na milele.
9:6 Kum 29:28; Yer 2:3; Mhu 9:5; Isa 14:22; 26:14; Sef 2:8-10; Za 34:16; 109:15Uharibifu usiokoma umempata adui,
umeingʼoa miji yao;
hata kumbukumbu lao limetoweka.