Zaburi 80:8-19
80:8 Isa 5:1-2, 7; Yer 2:21; Mt 21:33-41; Kut 15:17; 23:28-30; Yos 13:6; Mdo 7:45; Eze 15:6Ulileta mzabibu kutoka Misri,
ukawafukuza mataifa, ukaupanda.
Uliandaa shamba kwa ajili yake,
mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.
Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,
matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.
80:11 Kut 23:31; Za 72:8Matawi yake yalienea mpaka Baharini,80:11 Huenda inamaanisha Bahari ya Mediterania.
machipukizi yake mpaka kwenye Mto.80:11 Yaani Mto Frati.
80:12 Isa 5:5; 30:13; Za 89:40; Yer 39:8Mbona umebomoa kuta zake
ili wote wapitao karibu
wazichume zabibu zake?
80:13 Yer 5:6Nguruwe mwitu wanauharibu
na wanyama wa kondeni hujilisha humo.
80:14 Kum 26:15; Zek 1:12, 16, 17; Isa 63:15Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote!
Tazama chini kutoka mbinguni na uone!
Linda mzabibu huu,
80:15 Isa 49:5mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume,
mwana uliyemlea
kwa ajili yako mwenyewe.
80:16 Za 79:1; Kum 28:20Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto,
unapowakemea, watu wako huangamia.
80:17 Ay 25:6; Za 89:21; 110:1; Kut 4:22; Dan 7:13, 14; Yn 5:21-27Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume,
mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.
80:18 Za 85:6; Isa 57:15; Hos 6:2Ndipo hatutakuacha tena,
utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako.
80:19 Hes 6:25; Za 27:4, 9Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;
utuangazie uso wako,
ili tuweze kuokolewa.