Zaburi 73:15-28
Kama ningesema, “Nitasema hivi,”
ningelikuwa nimewasaliti watoto wako.
73:16 Mhu 8:17Nilipojaribu kuelewa haya yote,
yalikuwa magumu kwangu kuelewa.
73:17 Kut 15:17; Ay 8:13; Flp 3:19; Za 15:1; 77:13Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu,
ndipo nilipotambua mwisho wao.
73:18 Kum 32:35; Za 35:6; 17:13Hakika unawaweka mahali pa utelezi,
unawaangusha chini kwa uharibifu.
73:19 Kum 28:20; Mit 24:22; Isa 47:11; Mwa 19:15Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula,
wanatoweshwa kabisa na vitisho!
73:20 Za 78:65; Isa 29:8; Ay 20:8; Mit 12:11; 28:19Kama ndoto mtu aamkapo,
hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana,
utawatowesha kama ndoto.
Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa,
na roho yangu ilipotiwa uchungu,
73:22 Za 49:10; 92:6; 49:12, 20; Mhu 3:18; 9:12nilikuwa mpumbavu na mjinga,
nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.
73:23 Mwa 48:13Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote,
umenishika mkono wangu wa kuume.
73:24 Za 48:14; 1Fal 22:5; Isa 58:8; Yn 14:3; 2Kor 5:1Unaniongoza kwa shauri lako,
hatimaye utaniingiza katika utukufu.
73:25 Za 16:2; Flp 3:8Nani niliye naye mbinguni ila wewe?
Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.
73:26 Kum 32:9; Za 18:1; 84:2; 31:10; 40:12Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa,
bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu
na fungu langu milele.
73:27 Za 34:21; Law 6:2; Yer 5:11; Hos 4:12; 9:1Wale walio mbali nawe wataangamia,
unawaangamiza wote wasio waaminifu kwako.
73:28 Sef 3:2; Yak 4:8; Za 40:5; 26:7; 9:9; Ebr 10:22Lakini kwangu mimi,
ni vyema kuwa karibu na Mungu.
Nimemfanya Bwana Mwenyezi kimbilio langu;
nami nitayasimulia matendo yako yote.