Zaburi 72:1-20
Zaburi 72
Maombi Kwa Ajili Ya Mfalme
Zaburi ya Solomoni.
72:1 Kum 1:16; Za 9:8Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako,
mwana wa mfalme kwa haki yako.
72:2 Isa 11:2, 4, 5; 16:5; 9:7; Yer 23:5; 33:15Atawaamua watu wako kwa haki,
watu wako walioonewa kwa haki.
Milima italeta mafanikio kwa watu,
vilima tunda la haki.
72:4 Za 27:11; 76:9; 9:12; Isa 49:13; 11:4; 29:19; 32:7Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu
na atawaokoa watoto wa wahitaji,
ataponda mdhalimu.
72:5 1Sam 13:13; Za 33:11Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.
72:6 Kum 32:2Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa,
kama manyunyu yanyeshayo ardhi.
72:7 Za 92:12; Mit 14:11Katika siku zake wenye haki watastawi;
mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.
72:8 Kut 23:31; 1Fal 4:21; Zek 9:10Atatawala kutoka bahari hadi bahari
na kutoka Mto72:8 Yaani Mto Frati. mpaka miisho ya dunia.
Makabila ya jangwani watamsujudia,
na adui zake wataramba mavumbi.
72:10 Mwa 10:4, 7; Es 10:1; 1Fal 9:16; 2Nya 9:24Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali
watamletea kodi;
wafalme wa Sheba na Seba
watampa zawadi.
72:11 Mwa 27:29; Ezr 1:2Wafalme wote watamsujudia
na mataifa yote yatamtumikia.
Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia,
aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.
72:13 Isa 60:10; Yoe 2:18; Lk 10:33Atawahurumia wanyonge na wahitaji
na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.
72:14 Za 69:18; Eze 13:23; 34:10; 1Sam 26:21Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili,
kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.
72:15 Mwa 10:7; Za 35:28Aishi maisha marefu!
Na apewe dhahabu ya Sheba.
Watu wamwombee daima
na kumbariki mchana kutwa.
72:16 Eze 34:27; Isa 4:2; 27:6; 44:4; 58:11; 66:14; Mwa 27:18; Hes 22:4; Za 4:7; 92:12; 104:16Nafaka ijae tele katika nchi yote,
juu ya vilele vya vilima na istawi.
Tunda lake na listawi kama Lebanoni,
listawi kama majani ya kondeni.
72:17 Kut 3:15; Lk 1:48; Za 89:36; Mwa 12:3Jina lake na lidumu milele,
na lidumu kama jua.
Mataifa yote yatabarikiwa kupitia kwake,
nao watamwita aliyebarikiwa.
72:18 1Nya 29:10; Za 41:13; 106:48; Lk 1:68; Ay 5:9Bwana Mungu, Mungu wa Israeli, apewe sifa,
yeye ambaye peke yake hutenda mambo ya ajabu.
72:19 2Sam 7:26; Hes 14:21; Za 41:13Jina lake tukufu lisifiwe milele,
ulimwengu wote ujae utukufu wake.
Amen na Amen.
72:20 Rut 4:17Huu ndio mwisho wa maombi ya Daudi mwana wa Yese.