Zaburi 70:1-5
Zaburi 70
Kuomba Msaada
(Zaburi 40:13-17)
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.
70:1 Za 35:4; 6:10; 35:26; 71:12; 109:29; 129:5Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
70:2 Za 35:2Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
70:4 Za 31:6, 7; 35:27; 32:11; 118:24; 9:10Lakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Mungu na atukuzwe!”
70:5 Za 109:22; 141:1; 30:10; 86:1; 33:10; 18:2; 119:60Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
Ee Bwana, usikawie.