Zaburi 55:12-23
Kama aliyenitukana ni adui yangu, ningevumilia,
kama mtu mwovu angejiinua dhidi yangu,
ningejificha asinione.
55:13 2Sam 15:12Kumbe ni wewe, mwenzangu,
mshiriki na rafiki yangu wa karibu,
55:14 Mdo 1:16-17; Za 42:4ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri,
tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.
55:15 Za 64:7; 49:14; Mit 6:5; Isa 29:5; 47:9, 11; 1The 5:3; Hes 16:30Kifo na kiwajie adui zangu ghafula,
na washuke kuzimu wangali hai,
kwa maana uovu upo ndani yao.
Lakini ninamwita Mungu,
naye Bwana huniokoa.
55:17 Za 141:2; 88:13; 92:2; 5:3; Mdo 3:1; 10:9; 10:3, 30; Lk 18:1; Dan 6:10Jioni, asubuhi na adhuhuri
ninalia kwa huzuni,
naye husikia sauti yangu.
55:18 2Nya 32:7Huniokoa nikawa salama katika vita
vilivyopangwa dhidi yangu,
ingawa watu wengi hunipinga.
55:19 Kum 33:27; Za 29:10; 78:59; 36:1; 64:4; Kut 15:18Mungu anayemiliki milele,
atawasikia na kuwaadhibu,
watu ambao hawabadilishi njia zao,
wala hawana hofu ya Mungu.
55:20 Za 7:4; 41:9Mwenzangu hushambulia rafiki zake,
naye huvunja agano lake.
55:21 Za 59:7; 57:4; 12:2; 64:3; Ufu 1:16; Mit 5:3; 6:24; 12:18Mazungumzo yake ni laini kama siagi,
hata hivyo vita vimo moyoni mwake.
Maneno yake ni mororo kuliko mafuta,
hata hivyo ni upanga mkali uliofutwa.
55:22 1Pet 5:7; Za 15:5; 18:35; 112:6; 21:7; 37:24; Mt 6:25-34Mtwike Bwana fadhaa zako,
naye atakutegemeza,
hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
55:23 Za 5:6; 11:1; 9:15; 73:18; 94:13; 25:2; 30:3; 56:3; Isa 14:15; Eze 28:8; Lk 8:31; Ay 15:32Lakini wewe, Ee Mungu,
utawashusha waovu katika shimo la uharibifu.
Wenye kiu ya kumwaga damu na wenye hila,
hawataishi nusu ya siku zao.
Lakini mimi ninakutumaini wewe.