Zaburi 54:1-7
Zaburi 54
Kuomba Ulinzi Wa Mungu Kutokana Na Adui
Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?”
54:1 1Sam 24:15; 20:1; 2Nya 20:6Ee Mungu uniokoe kwa jina lako,
unifanyie hukumu kwa uwezo wako.
54:2 Za 4:1; 5:1; 55:1Ee Mungu, sikia maombi yangu,
usikilize maneno ya kinywa changu.
54:3 Za 36:1; 86:14; 18:48; 140:1, 4, 11; 1Sam 20:1Wageni wananishambulia,
watu wakatili wanayatafuta maisha yangu,
watu wasiomjali Mungu.
54:4 1Nya 5:20; Za 20:2; 18:35; Isa 41:10; Ebr 13:6; Rum 8:31, 32Hakika Mungu ni msaada wangu,
Bwana ndiye anayenitegemeza.
54:5 Kum 32:35; Isa 42:3; Mit 24:12; Za 89:49; 94:23Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia,
kwa uaminifu wako uwaangamize.
54:6 Law 7:12, 16; Ezr 1:4; Za 27:6; 44:8; 52:9; 138:2; 142:7; 145:1; 69:30Nitakutolea dhabihu za hiari;
Ee Bwana, nitalisifu jina lako
kwa kuwa ni vyema.
Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote,
na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.